#235
Tumekombozwa katika nchi
Wokovu
Couplet 1
Tumekombozwa katika nchi, usikilize vema, rafiki! :/: Tumeokoka tufike juu, taji kutiwa, furaha kuu! :/:
Couplet 2
Tumekombozwa katika watu, hata tuchekwe kitambo huku. :/: Twavumilia katika shida, twatazamia ’heri wa Mbingu. :/:
Couplet 3
Tumekombozwa, tuwe wa huru, tukichokozwa haitudhuru. :/:Tutaondoka, ’hamia Mbingu, tutasimama mbele ya Mungu.:/:
Couplet 4
Tumekombozwa, furaha kuu, twaandaliwa karamu kuu! :/: Salamu hiyo uitangaze, wafike mbio na waokoke! :/:
Couplet 5
E’ mama, baba, mbona kungoja? Ndugu na dada, fika pamoja! :/: Mwenye kukawa hataingia, leo waitwa na Yesu pia. :/: