Indirimbo Zikundwa Open in the app

#233

Tazama Mwokozi aliyekufilia

Wokovu

Couplet 1

Tazama Mwokozi aliyekufilia ili wewe upate uzima! Tazama, kwa pendo atakusaidia, usidumu dhambini daima!

Refrain

Yainue macho! Tazama Mwokozi aliyekufilia, ili upate uzima!

Couplet 2

Mwokozi alisulibiwa ju’ ya mti ili sisi tupate Wokovu. Alitukomboa kwa Damu yake safi, kwate yeye twapata wongofu.

Refrain

Yainue macho! Tazama Mwokozi aliyekufilia, ili upate uzima!

Couplet 3

Hakuna majuto yaweza’ kutuponya, ila Damu ya Yesu Masiya. Ufike kwa Yesu apate kukuonya jinsi yaondokavyo hatia!

Refrain

Yainue macho! Tazama Mwokozi aliyekufilia, ili upate uzima!

Couplet 4

Rafiki, waitwa na Mungu kwa Wokovu, anataka ufike upesi. Kwa nini kukawa, ufike bila hofu, uondoke katika hatari!

Refrain

Yainue macho! Tazama Mwokozi aliyekufilia, ili upate uzima!

Couplet 5

Ufike, pokea uzima wa milele, Bwana Yesu ali’tuletea! Karama ya Mbingu ni tumaini letu, ipokee na hutapotea!

Refrain

Yainue macho! Tazama Mwokozi aliyekufilia, ili upate uzima!