#232
Nilipofika kwa Bwana Yesu
Wokovu
Couplet 1
Nilipofika kwa Bwana Yesu, nikapaaza sauti yangu: "Yesu Mwokozi, unirehemu!" Akaniokoa. :/: Yesu asifiwe! :/: Alisikia kilio changu, Yesu asifiwe!
Couplet 2
Nilipofika kwa Bwana Yesu, nikamsihi Mwokozi wangu: "Unitakase, nifanye safi!" Akanisikia. :/: Yesu asifiwe. :/: Alisikia maombi yangu, Yesu asifiwe!
Couplet 3
Ona kisima cha Msalaba, leo kingali chabubujika kuniokoa na kusafisha! Yesu asifiwe! :/: Yesu asifiwe:/: Aniokoa, anisafisha, Yesu asifiwe!
Couplet 4
Njoo kwa Yesu, kisima hicho, unywe, uoshwe katika maji! Kiu yapoa, na watakaswa, Yesu asifiwe. :/: Yesu asifiwe! :/: Kiu yapoa, na watakaswa, Yesu asifiwe!