Indirimbo Zikundwa Open in the app

#231

Mwokozi alitoa Damu kwa’jili...

Wokovu

Couplet 1

Mwokozi alitoa Damu kwa’jili ya waovu, Msalabani alikufa kuniokoa mimi.

Refrain

E’ Yesu, niokoe sana, nifunze kuamini! Na unilinde tena, Bwana, nisipotee kamwe!

Couplet 2

Alijitwika dhambi zetu, huzuni na maradhi; Neema kubwa, wema wingi, upendo wa ajabu!

Refrain

E’ Yesu, niokoe sana, nifunze kuamini! Na unilinde tena, Bwana, nisipotee kamwe!

Couplet 3

Na hapo jua likafichwa, ikawa giza kuu; muumba alitufilia kutulipia deni.

Refrain

E’ Yesu, niokoe sana, nifunze kuamini! Na unilinde tena, Bwana, nisipotee kamwe!

Couplet 4

Magoti yangu nayapiga Msalabani pake, na kwa machozi natazama mateso yake huko.

Refrain

E’ Yesu, niokoe sana, nifunze kuamini! Na unilinde tena, Bwana, nisipotee kamwe!

Couplet 5

Nitakurudishia nini, Mwokozi wangu Mwema? E’ Bwana, nikutumikie maisha yangu yote!