#227
Mungu aliye Mbinguni
Wokovu
Couplet 1
Mungu aliye Mbinguni alitupa kiongozi, naye ni rafiki wa watoto wote. Ukijua jina lake, ulitaje sasa hivi! Anapenda wote, hata wewe, nami.
Refrain
Mbingu na ufalme wake wa wototo wote sasa! Mbio tuishike njia iendayo kwake Yesu ili tuione raha ya Mbinguni!
Couplet 2
Yesu mwenye Pendo kubwa awakumbatia wote, anawabariki kwa huruma yake. Hatuoni huku chini mtu Mwema kama yeye, hasahau mtu, hata mnyang’angyi.
Refrain
Mbingu na ufalme wake wa wototo wote sasa! Mbio tuishike njia iendayo kwake Yesu ili tuione raha ya Mbinguni!
Couplet 3
Yesu ni Mchunga Mwema, anawakusanya sasa mkononi mwake wana wa kondoo. Kifuani mwake tena anawachukua wote hata kwa ufalme wake huko juu.
Refrain
Mbingu na ufalme wake wa wototo wote sasa! Mbio tuishike njia iendayo kwake Yesu ili tuione raha ya Mbinguni!