Indirimbo Zikundwa Open in the app

#228

Wakati wa utoto wako

Wokovu

Couplet 1

Wakati wa utoto wako, hujapoona shida bado, sauti ilikuambia: "Unipe sasa moyo wako!"

Refrain

Wajua ni nani huyu anayekuita sasa? Ni Yesu, rafiki yako; anakuita: " Njoo kwangu!"

Couplet 2

Na katika ujana wako wausikia mwito wake, na jinsi utakavyoshinda Shetani akikujaribu.

Refrain

Wajua ni nani huyu anayekuita sasa? Ni Yesu, rafiki yako; anakuita: " Njoo kwangu!"

Couplet 3

Wakati wa uzee wako dhambini ukiendelea hata kukaribia kufa, Mwokozi akuita tena.

Refrain

Wajua ni nani huyu anayekuita sasa? Ni Yesu, rafiki yako; anakuita: " Njoo kwangu!"