#222
Bwana Yesu anasema, Dhaifu wewe
Wokovu
Couplet 1
Bwana Yesu anasema: "Dhaifu wewe sana. Mimi ni mchunga Mwema". Na kwa hiyo namwandama.
Refrain
Yesu alikufa kwa ajili yangu, aliziondoa dhambi, furaha kubwa kwangu!
Couplet 2
Pendo la Mwokozi wangu limeyeyusha moyo. Ametoa dhambi zangu na kiburi na uchoyo.
Refrain
Yesu alikufa kwa ajili yangu, aliziondoa dhambi, furaha kubwa kwangu!
Couplet 3
Sina kitu mkononi cha kunifaidia; udhaifu u moyoni, Yesu ninamlilia.
Refrain
Yesu alikufa kwa ajili yangu, aliziondoa dhambi, furaha kubwa kwangu!
Couplet 4
Mungu akisaidia nitamaliza mwendo. "Yesu alinifilia", nitaimba huko ng’ambo.
Refrain
Yesu alikufa kwa ajili yangu, aliziondoa dhambi, furaha kubwa kwangu!
Couplet 5
Siku moja nitafika Mbinguni huko juu, nitaimba kadhalika shukrani kuu.