Indirimbo Zikundwa Open in the app

#223

Ni uheri bora kumwamini Bwana

Wokovu

Couplet 1

Ni uheri bora kumwamini Bwana Yesu kwa wakati wa ujana wetu, kabla hatujazionja dhambi na mashaka zinazoharibu roho zetu.

Refrain

Ni uheri bora kumwamini Bwana Yesu, na kumfuata kila siku. Na ujana wetu ukitukimbia tena, shangwe ya Wokovu itabaki.

Couplet 2

Ni uheri bora kumtii Bwana Yesu kwa wakati wa ujana wetu. Hivyo tutakuwa na dhamiri safi, njema kwa maisha yetu yote pia.

Refrain

Ni uheri bora kumwamini Bwana Yesu, na kumfuata kila siku. Na ujana wetu ukitukimbia tena, shangwe ya Wokovu itabaki.

Couplet 3

Ni uheri bora kumtumikia Yesu kwa wakati wa ujana wetu. Bwana Yesu akumbuka kila tendo dogo, atalipa kwa Neema yake.

Refrain

Ni uheri bora kumwamini Bwana Yesu, na kumfuata kila siku. Na ujana wetu ukitukimbia tena, shangwe ya Wokovu itabaki.

Couplet 4

Ni uheri bora kumngoja Bwana Yesu kwa wakati wa ujana wetu. Atatuchukua kwake kwa furaha kubwa, tutakuwa naye siku zote.