Indirimbo Zikundwa Open in the app

#216

Nafasi ingaliko Arusini

Wokovu

Couplet 1

Nafasi ingaliko Arusini ita’yokuwa kwake Mungu Baba. Njoo kwake, nafasi ingaliko!

Couplet 2

Njiani mwako jua linakuchwa, jioni inakaribia sasa. Njoo mbio, nafasi ingaliko!

Couplet 3

Karamu ya arusi ni tayari, na Bwana anakualika wewe. Njoo mbio, nafasi ingaliko!

Couplet 4

Wanaingia watu wengi huko, ufanye hima, uingie nawe! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

Couplet 5

Tazama, lango limefunguliwa, Neema gani: Utakaribikshwa! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

Couplet 6

Ufike mbio, utaona heri, Yesu atoa wingi wa neema! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

Couplet 7

Je, utaona shangwe ya Mbinguni? Bwana arusi akungoja sana. Njoo mbio, nafasi ingaliko!

Couplet 8

Uliyesitasita unaitwa, ujiazimu kuja kwake Mungu! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

Couplet 9

Ukichelewa, lango litafungwa, na utalisikia neno hili: "Ondokeni! Sikuwajua ninyi!"