Indirimbo Zikundwa Open in the app

#215

Mwenyezi Mungu anafanya ishara

Wokovu

Couplet 1

Mwenyezi Mungu anafanya ishara kubwa duniani, anaondoa minyororo inayofunga watu huku. Avunja nyavu za shetani, na wakosaji waokoka.

Couplet 2

Maneno yake yana nguvu kushinda yote ya zamani. Na watu wanapiga mbio kuomba ne’ma ya Mwokozi. Wakiyapata masamaha, waimba wote: "Sifu Mungu!"

Couplet 3

Tazama, ndugu wengi sana wanafuata Yesu leo; katika kila nchi sasa maelfu wanapenda Mungu. Wengine wanavutwa naye Mwenyezi Mungu, Baba yetu.

Couplet 4

Inua macho, mvunaji, mavuno yanaiva sana! Uende kutafuta watu, uwapeleke kwake Yesu! E’ ndugu wote, amkeni, ’kawaokowe wenye dhambi!

Couplet 5

Wengine wanapoingia ufalme wako, Yesu Kristo, nisibakie huku chini, Neema hiyo nakuomba! Nakaa mikononi mwako, unifikishe huko kwako!

Couplet 6

Najua siku ni karibu Mwokozi atakaporudi, awachukue watu wake mpaka nchi ya amani. E’ siku ya uheri bora, nakutamani. Uje mbio.