Indirimbo Zikundwa Open in the app

#214

Namtafuta mwana wangu

Wokovu

Couplet 1

Namtafuta mwana wangu, mtoto yu wapi leo? Alienifurahisha mbele, ningali ninampenda.

Refrain

Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu, urudi, ninakutafuta, mwanangu, mpendwa wangu!

Couplet 2

Uliyekuwa safi sana katika utoto wako, uliichafua roho yako kwa dhambi na njia mbaya.

Refrain

Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu, urudi, ninakutafuta, mwanangu, mpendwa wangu!

Couplet 3

Ninatamani kukuona katika usafi tena, na kukusikia ukiomba na kumshukuru Yesu.

Refrain

Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu, urudi, ninakutafuta, mwanangu, mpendwa wangu!

Couplet 4

Nitafutie mpotevu kwa pendo na tumaini! Unisalimie mwana wangu, ya kwamba ninamngoja!