Indirimbo Zikundwa Open in the app

#212

Sauti ya Yesu niliisikia, kwa pendo

Wokovu

Couplet 1

Sauti ya Yesu niliisikia, kwa pendo aliniambia: "Ufike, nataka kukusaidia, nangoja, nangoja, ufike!"

Refrain

Njoo kwa Yesu, ufike upesi, uupokee Wokovu wa Mungu! Mbona kukawa dhambini, rafiki? Yesu anakuita, njoo!

Couplet 2

Ukiwa na hofu kufika kwa Yesu, uliye na dhambi rohoni, kumbuka ya kuwa huruma ni tele; ufike kwa Yesu, angoja!

Refrain

Njoo kwa Yesu, ufike upesi, uupokee Wokovu wa Mungu! Mbona kukawa dhambini, rafiki? Yesu anakuita, njoo!

Couplet 3

Ukiwa maskini, dhaifu kabisa, Mwokozi anakufahamu. Anakuambia: " Pokea neema, uache mzigo wa dhambi!"

Refrain

Njoo kwa Yesu, ufike upesi, uupokee Wokovu wa Mungu! Mbona kukawa dhambini, rafiki? Yesu anakuita, njoo!

Couplet 4

Na kama nilivyo ninamfikia Mwokozi aliyenipenda. Ninaupokea Wokovu na raha; kwa shangwe ninamshukuru!