Indirimbo Zikundwa Open in the app

#211

Njoo kwa Yesu usishangae

Wokovu

Couplet 1

Njoo kwa Yesu, usishangae! Akuonyeshe njia ya Mbingu. Msikilize, anakusihi: Mtu wa dhambi, njoo!

Refrain

Heri, heri, tutakusanyika kwake Mungu kwa furaha kuu! Shida na shaka hazitakuwa kwetu Mbinguni juu.

Couplet 2

Yesu aita, wote wafike, atatuliza wenye huzuni, kuwatolea pendo na raha. Usikiaye, njoo!

Refrain

Heri, heri, tutakusanyika kwake Mungu kwa furaha kuu! Shida na shaka hazitakuwa kwetu Mbinguni juu.

Couplet 3

Sasa wakati wakuokoka, uje upesi, umkubali! Mwenye amsikitiko na dhambi, njoo kwa Yesu sasa!

Refrain

Heri, heri, tutakusanyika kwake Mungu kwa furaha kuu! Shida na shaka hazitakuwa kwetu Mbinguni juu.