#208
Piga makengele ya furaha leo
Wokovu
Couplet 1
Piga makengele ya furaha leo kwa sababu mtu ametubu! Mwana mpotevu amerudi sasa, baba amemsamehe yote.
Couplet 2
Nyimbo za furaha ya Mbinguni, Nyimbo za furaha ya Wakristo! Tuna’sifu Mungu kwa sababu sasa mtu huyu amwamini Yesu.
Couplet 3
Piga makengele, ni furaha nyingi; mkosaji amefunguliwa! Yesu alivunja minyororo yake, alimpa roho ya kimwana.
Couplet 4
Piga makengele! Hiyo ni habari yakupasha mbali na karibu. Mtu amepata kuwa mtu mpya, dhambi zake zimeondolewa!