#207
Umgeukie Mwokozi, jitenge na ovu
Wokovu
Couplet 1
Umgeukie Mwokozi, jitenge na ovu na dhambi! Babako angoja ufike; usiangamie milele!
Couplet 2
Kijana, unafurahia maisha na mambo ya nchi. Baada ya muda kitambo utahukumiwa na Mungu.
Couplet 3
Kwa nini kujiangamiza katika tamaa za huku? Usijipoteze dhambini! Dunia isikuharibu!
Couplet 4
Umkimbilie Mwokozi, atakupokea kwa pendo, na utaokoka hakika kwa nguvu ya Damu ya Yesu!
Couplet 5
Walio Mbinguni waimba, wanayo mavazi meupe; hutaki sehemu pamoja na wao nyumbani mwa Baba?
Couplet 6
Je, mwisho utaona wapi mahali pa kujisitiri? Dunia itakapochomwa utakosa makimbilio.
Couplet 7
Ujipatanishe na Mungu, na usichelewe, rafiki! Ukimkataa Mwokozi, utatupwa nje gizani.
Couplet 8
Chagua pasipo kukawa! Mwokozi atakupokea. Angoja ufike kutubu; atakutakasa kwa Damu.