Indirimbo Zikundwa Open in the app

#209

Uwatafute wanaopotea

Wokovu

Couplet 1

Uwatafute wanaopotea, na kwa upendo watoe dhambi! Lia pamoja na wenye huzuni, uwapeleke kwa Yesu Mwokozi!

Refrain

Uwatafute wanaopotea! Yesu Mwokozi awahurumia.

Couplet 2

Anatafuta waliokimbia, anawangoja warudi upesi. Uwafundishe kwa pendo na kweli ju’ ya Neema na haki ya Yesu!

Refrain

Uwatafute wanaopotea! Yesu Mwokozi awahurumia.

Couplet 3

Ndani ya roho na katika siri labda waona shauku ya Mungu. Uwaongoze kwa Yesu Mwokozi, wafahamishe upendo wa Mungu!

Refrain

Uwatafute wanaopotea! Yesu Mwokozi awahurumia.

Couplet 4

Uwatafute wanaopotea! Mungu atoa upendo na nguvu. Uwapeleke kwa Yesu mpozi, Mwenye huruma na afya kwa wote!

Refrain

Uwatafute wanaopotea! Yesu Mwokozi awahurumia.