Indirimbo Zikundwa Open in the app

#206

Rafiki yangu tazama

Wokovu

Couplet 1

Rafiki yangu, tazama, wapita njia ya wapi? Milele, je? utakaa wapi ukikataa Mungu?

Refrain

Ujiandae sasa, utakutana na Mungu! Lazima uwe tayari kwa sababu utamuona!

Couplet 2

Dunia haina raha, amani wala salama. Fahari yake ikikuloga, utapotea njia.

Refrain

Ujiandae sasa, utakutana na Mungu! Lazima uwe tayari kwa sababu utamuona!

Couplet 3

Lo! Yesu anakuita! Kwa nini unachelewa? Ushike njia ufike kwake! Ataja jina lako.

Refrain

Ujiandae sasa, utakutana na Mungu! Lazima uwe tayari kwa sababu utamuona!

Couplet 4

Uache haya na hofu, Mwokozi anakupenda! Kwa Damu alikomboa wewe, anakutaka sasa.

Refrain

Ujiandae sasa, utakutana na Mungu! Lazima uwe tayari kwa sababu utamuona!

Couplet 5

Ikiwa unachelewa kupatanishwa na Mungu, utamkuta Mwokozi kama mwamuzi mwenye haki.