#205
Yesu Mwokozi aita kwa pendo
Wokovu
Couplet 1
Yesu Mwokozi aita kwa pendo mimi na wewe na wote, na yu karibu kukukaribisha wewe uliye dhambini.
Refrain
Urudi, urudi, Sasa urudi kwa Yesu! Anakuita na anakungoja. Leo urudi kwa Yesu!
Couplet 2
Mbona kukawa anapokuita? Anakungoja, ufike! Kuna nafasi karibu na Yesu; njia ni wazi kwa wote.
Refrain
Urudi, urudi, Sasa urudi kwa Yesu! Anakuita na anakungoja. Leo urudi kwa Yesu!
Couplet 3
Nyakati zetu zapita upesi, hazitarudi kabisa. Njoo kwa Yesu upate amani, leo ungali mzima!
Refrain
Urudi, urudi, Sasa urudi kwa Yesu! Anakuita na anakungoja. Leo urudi kwa Yesu!
Couplet 4
Ona upendo mkubwa wa Yesu, unaenea kwa wote! Na kwa Neema anakukumbuka wewe na mimi na wote.
Refrain
Urudi, urudi, Sasa urudi kwa Yesu! Anakuita na anakungoja. Leo urudi kwa Yesu!