#199
Njoni wote mteswao!
Wokovu
Couplet 1
Njoni wote mteswao! Wote wenye sikitiko kwa ajili ya makosa, mje sasa kwa Mwokozi! Kwake mtaona raha, utulivu na amani. Matulizo mioyoni mtapata kwake Yesu.
Couplet 2
Hataacha sikitiko kulemea moyo wako; Yesu ni mchunga Mwema, akuficha mazizini. Pendo lake lina nguvu, huchukua masumbuko, hufariji roho yako, hukutwaa kwake Mungu.
Couplet 3
Yesu kama nyota nzuri ing’aayo asubuhi, mtu amfuataye ataona njia wazi. hata nyota za Mbinguni zikiteketea zote, nyota hiyo ya milele haitazimika kamwe.