Indirimbo Zikundwa Open in the app

#200

Njoni wote, mle, mnywe

Wokovu

Couplet 1

Njoni wote, mle, mnywe, Yesu anasema hivyo. "Nimetoa mwili wangu kwa ajili yenu ninyi." Kila mtu mwenye njaa aje na apate kula! Na aliye na makosa atasamehewa yote.

Couplet 2

Ninakuja kwako, Yesu, unithibitishe moyo! Uliona umaskini, niwe mwenye uta-jiri. Nishibishe mema yako na karama takatifu! Unijaze Roho yako kama ulivyoahidi!

Couplet 3

Yesu, ninakuja kwako niungane nawe, Bwana! Mimi mwenye udhaifu, nakutegemea wewe. Na kwa Damu yako, Yesu, ninatakasika sasa. Nashiriki mwili wako katika agano jipya.