Indirimbo Zikundwa Open in the app

#198

E’ mtu mwenye kiu, ufike kwake

Wokovu

Couplet 1

E’ mtu mwenye kiu, ufike kwake Yesu, :/: upate maji ya uzima, hutaona kiu kamwe! :/:

Refrain

Njoo kwa Yesu, uyanywe maji hai! Ufike, na utapewa uzima na uhodari!

Couplet 2

Na tazama, ndugu wengi wamekwisha kunywa! :/: Ni heri kubwa, maji hayo hayatakauka kamwe! :/:

Refrain

Njoo kwa Yesu, uyanywe maji hai! Ufike, na utapewa uzima na uhodari!

Couplet 3

Na wewe unywe pia, upate nguvu sana! :/: Tumia katika shindano upanga wa neno lake! :/:

Refrain

Njoo kwa Yesu, uyanywe maji hai! Ufike, na utapewa uzima na uhodari!

Couplet 4

Na mwendo wa imani uta’poumaliza, :/: utayakunywa maji bora mkwa Mungu Mbinguni juu. :/:

Refrain

Njoo kwa Yesu, uyanywe maji hai! Ufike, na utapewa uzima na uhodari!