Indirimbo Zikundwa Open in the app

#197

Hapo nilipokuwa dhambini

Wokovu

Couplet 1

Hapo nilipokuwa dhambini, niliumwa kwatika roho. Sasa ninafurahi kwa shangwe kwani Yesu ameniponya.

Refrain

Ndiyo kazi kubwa ya ajabu: Mwokozi aliniokoa! Naye anapenda watu wote, atakuokoa wewe.

Couplet 2

Dhambi zote nilizozitenda zimefutwa na Bwana Yesu. Sikitiko kwa ’jili ya dhambi zilikoma nilipotubu.

Refrain

Ndiyo kazi kubwa ya ajabu: Mwokozi aliniokoa! Naye anapenda watu wote, atakuokoa wewe.

Couplet 3

Sasa mimi sitaki kurudi, nachukia kabisa dhambi. Nimeonja furaha ya Mungu na amani na raha yake.

Refrain

Ndiyo kazi kubwa ya ajabu: Mwokozi aliniokoa! Naye anapenda watu wote, atakuokoa wewe.