#192
Sauti moja iliniuliza
Wokovu
Couplet 1
Sauti moja iliniuliza: " Wajua nilikufanyia nini? :/: Kwa’jili yako niliteswa sana; ufike kwangu, kwani nakupenda! " :/:
Couplet 2
" Nilipokuwa huku duniani wakanitia taji ya miiba, :/: Na sikupambwa fedha na dhahabu, lakini majeraha na uchungu." :/:
Couplet 3
" Golgotha nilifika siku moja, na nilikufa ju’ ya Msalaba. :/: Tazama, katika mikono yangu nimekuchora, e’ mtoto wangu. ":/:
Couplet 4
Haleluya, rohoni ninaimba! Nimejiweka mikononi mwake. :/: Na Yesu ananiongoza sasa, nifike nchi nzuri huko juu. :/: