Indirimbo Zikundwa Open in the app

#191

Yapigwa hodi kwangu mgeni afika

Wokovu

Couplet 1

Yapigwa hodi kwangu, mgeni a’fika, akiniomba: "Nifungulie! Umande umeshuka kichwani usiku, na nywele zangu zimelowa maji".

Couplet 2

A! Huyu si mgeni, ni Yesu Mwokozi, sauti yake nzuri na’jua. Ninamfungulia, naona ni Yesu; na siku hiyo sitaisahau.

Couplet 3

Anong’oneza sasa rohoni: "U wangu", karibu naye ninatulia. Ananitia nguvu, baraka ya Mbingu; daima nitakaa kwake Yesu.

Couplet 4

Ni kweli, mimi ni wa Mwokozi milele, amenitaja: "Ndugu, mpenzi". Ananikarimia hazina za Mbingu, ninaingoja siku ya arusi.