#193
Ni neno zuri la ’aminiwa
Wokovu
Couplet 1
Ni neno zuri la ’aminiwa, listahililo kukubaliwa, ya kwamba Yesu alitujia awaokoe wenye makosa.
Couplet 2
Wa kwanza mimi wa wenye dhambi, lakini ninafurahi sasa sababu Yesu, Mwokozi wangu, aliniosha kwa Damu yake.
Couplet 3
Mwokozi wetu yu nasi hapa, atenda kazi kwa nia yake; awasha Moto rohoni mwetu, uwezo gani utampinga?
Couplet 4
Viziwi wanasikia sasa, viwete wanatembea sawa, wenye ukoma watakasika, Injili yake yahubiriwa.
Couplet 5
E’ Bwana Yesu, tupulizie, tujaze Roho Mtakatifu! Uwaamshe waliokufa katika dhambi, uwaangaze!
Couplet 6
Fungua Mbingu unyeshe mvua panapo kiu na jangwa tupu! Uligeuze, likachanue na kufurahi kwa shangwe kuu!
Couplet 7
Na mataifa wakusujudu mahali pako patakatifu! Amina. Wako ni utukufu na sifa zote! Haleluya!