Indirimbo Zikundwa Open in the app

#190

Kisima cha lehi kingali

Wokovu

Couplet 1

Kisima cha lehi kingali kwa kila aliye na kiu. Kinatoa maji mazima yaliyo ya kuburudisha.

Refrain

Kisima chema cha maji safi hakikauki hata milele. Ni heri yangu, napumzika, na roho yangu inatulia.

Couplet 2

Ulie na kiu rohoni, ukinyong’onyea njiani, tazama kisima jangwani kilicho na afya, uzima!

Refrain

Kisima chema cha maji safi hakikauki hata milele. Ni heri yangu, napumzika, na roho yangu inatulia.

Couplet 3

Mtungi ukiwa mtupu, ukipungukiwa imani, ufike kisima cha maji yabubujikayo daima!

Refrain

Kisima chema cha maji safi hakikauki hata milele. Ni heri yangu, napumzika, na roho yangu inatulia.

Couplet 4

Na penye kisima cha lehi upange na kupumzika! Uketi kivulini mwake, na moyo utaburudishwa!