#181
Tutazame kule mbele
Wokovu
Couplet 1
Tutazame kule mbele, asubuhi inakuja! Tuamini Mungu wetu, atafanya kazi yake, kufukuza mashetani, kumiliki nchi yote. Tutashinda tukiomba, Mungu anatusikia.
Couplet 2
Tarumbeta linalia, tuamke wote sasa! Mungu wetu anataka sisi sote tutakaswe! Kila mtu awe safi katika kanisa lake! Uliache nung’uniko, utapata nguvu yake!
Couplet 3
Imba ninyi, watu wake, Bwana yu pamoja nasi! Tutashinda majaribu kwa uwezo wake Yesu. Twende tumhudumie kwa kumpa mali yake; hata roho na akili zimtumikie Bwana!
Couplet 4
Watu wengi hawajui njia yakufika Mbingu, wanakuwa wamefungwa kwa mikono ya shetani. Twende tukawatafute, tuwavute kwa Mwokozi, na kuomba na kukesha hata kuja kwake Yesu!