Indirimbo Zikundwa Open in the app

#182

Kisa cha kale nipe habari

Wokovu

Couplet 1

Kisa cha kale nipe, habari ya Mbinguni, ya Bwana Mtukufu, ya pendo lake Yesu! Niambie neno lake, nipate kusikia, mnyonge mimi huku, mjinga, mkosaji.

Refrain

Kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, cha pendo lake Yesu!

Couplet 2

Sema kwa taratibu nipate kuelewa habari ya Wokovu na Damu ya Mwokozi! Simulia mara nyingi, nisije kasahau, niikumbuke tena maisha yangu yote!

Refrain

Kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, cha pendo lake Yesu!

Couplet 3

Taja habari hiyo kwa wema na kwa pendo, Mwokozi alikufa kutukomboa sote. Na ikiwa unataka kunifariji mimi, nisimulie ile habari ya zamani!

Refrain

Kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, cha pendo lake Yesu!

Couplet 4

Nipe habari hiyo ikiwa waniona ninaipendelea fahari ya dunia! Siku nitakapo kufa ’tapenda kusikia habari ya zamani: Mponyi Mwema Yesu.

Refrain

Kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, cha pendo lake Yesu!