#180
Bwana Yesu anatuuliza
Wokovu
Couplet 1
Bwana Yesu anatuuliza: "Nimtume nani mavunoni? Watu wenye dhambi wapotea, watolee Neno la neema! "
Refrain
"Mungu wangu, sema nami! Uniguze sasa kwa makaa! Mungu wangu, sema nami! Mimi hapa, unitume sasa!"
Couplet 2
Mtumishi wake Bwana Mungu alisema: "Mimi sistahili". Aliposikia Moto safi, akasema: "Unitume mimi"!
Refrain
"Mungu wangu, sema nami! Uniguze sasa kwa makaa! Mungu wangu, sema nami! Mimi hapa, unitume sasa!"
Couplet 3
Mataifa mengi wanakufa, hawajui Yesu na Wokovu.Twende kwao mbio, tuhubiri neno la Wokovu wake Yesu!
Refrain
"Mungu wangu, sema nami! Uniguze sasa kwa makaa! Mungu wangu, sema nami! Mimi hapa, unitume sasa!"
Couplet 4
Siku za mavuno zitapita, watumishi watarudi kwao. Bwana wao atawapokea na kusema: "Ulifanya vema"!