Indirimbo Zikundwa Open in the app

#179

Siku moja mavuno yataisha kabisa

Wokovu

Couplet 1

Siku moja mavuno yataisha kabisa, baada ya hayo hukumu. Jua litazimika siku hiyo ya mwisho, na hutasikia injili.

Refrain

Atakusanya ngano kwa furaha ghalani, bali makapi yote yatatupwa Motoni. Rafiki, utakuwa wapi?

Couplet 2

Mahubiri na nyimbo za Wokovu wa Mungu zitakaponyamanza huku, uliyelikataa neno zuri la Mungu, utakaa wapi milele?

Refrain

Atakusanya ngano kwa furaha ghalani, bali makapi yote yatatupwa Motoni. Rafiki, utakuwa wapi?

Couplet 3

Watu wote wa Mungu wafikapo Mbinguni kukaa pamoja na Yesu, wataimba kabisa kwa sauti ya nguvu kumshangilia Mwokozi.

Refrain

Atakusanya ngano kwa furaha ghalani, bali makapi yote yatatupwa Motoni. Rafiki, utakuwa wapi?