Indirimbo Zikundwa Open in the app

#171

Mwenyezi Mungu ngome kuu

Wokovu

Couplet 1

Mwenyezi Mungu ngome kuu, silaha ya imara! Katika shida na huzuni twategemea yeye. Mwovu akitukaribia kututia woga, akijithibitisha kwa hila na jeuri, tusimwogope yeye!

Couplet 2

Kwa nguvu yetu tu dhaifu, na tungeshindwa hima, ila Mwenyezi yupo nasi, twaambatana naye. Ukitaka jina lake, ndilo Yesu Kristo; aliye mshindaji na mwenye mamlaka, Mfalme wa milele.

Couplet 3

Na dunia yote ikijaa majeshi ya giza, tuliye naye Mungu wetu, hatutaona hofu. Mwovu amehukumiwa, hana nguvu tena ya kutuangamiza maungo wala robo; ashindwa na Mwenyezi.

Couplet 4

Maneno yake Mungu wetu, tushikamane nayo! Hatushindii vya dunia, vya juu twatafuta. Tu hodari siku zote, hata hatarini; uzima twauweka kutii Mungu wetu: Ufalme una yeye.