#170
Nikiona shida huku katika safari
Wokovu
Couplet 1
Nikiona shida huku katika safari, Yesu aninong’oneza neno la faraja. Ananipa raha tele na furaha ya ajabu. Ninaandamana naye sasa na milele.
Couplet 2
Tena njia ikienda juu ya milima, ninakaribia Mbingu, nuru inaang’aa. Na katika nuru hii ninaona kwa uwazi nchi ya ahadi yake na urithi wangu.
Couplet 3
Kwa imani ninaimba, hata hatarini, njia ’kiwa ndefu huku, nitavumilia. Nyota za ahadi zake zinang’aa kwa usiku, zinaniongoza vema hata huko juu.
Couplet 4
Kama Musa aliona nchi ya ahadi, kadhalika natazama nchi yangu juu; ninaisalimu sasa hwa uheri na imani. Natamani kufikako, kwa urithi wangu.
Couplet 5
Vya hatari vikifika kati’ njia tena, Yesu yu pamoja nami, anichunga vema. Ninaendelea mbele, na Mbinguni nifikapo nyimbo nzuri nitaimba na Wakristo wote.