#172
Sisi tu viungo vya mwili ’moja
Wokovu
Couplet 1
Sisi tu viungo vya mwili ’moja, tunasaidiana. Utumishi wetu tunaupenda na twasaidiana.
Refrain
Twasaidiana sote, twasaidiana sote. Twamaliza kwa shangilio na kwa bidii kazi yetu.
Couplet 2
Twafurahi kwa utumishi, hata tukiwa peke yetu; walakini heri zaidi kama tukisaidiana.
Refrain
Twasaidiana sote, twasaidiana sote. Twamaliza kwa shangilio na kwa bidii kazi yetu.
Couplet 3
Ikiwezekana kwa mchwa ’dogo kujenga kisuguu, sisi nasi kwa nguvu yake Mungu tutamaliza kazi.
Refrain
Twasaidiana sote, twasaidiana sote. Twamaliza kwa shangilio na kwa bidii kazi yetu.
Couplet 4
Na umoja wetu ni wa thamani, unapendeza Mungu; anatubariki kwa neema, anatupa tunu kubwa.
Refrain
Twasaidiana sote, twasaidiana sote. Twamaliza kwa shangilio na kwa bidii kazi yetu.
Couplet 5
Twakuomba, Bwana, ’tuunganishe, tujaze Pendo lako! Na kwa Roho yako utubatize, tuhudumie wewe!