Indirimbo Zikundwa Open in the app

#164

Israeli wake Mungu, kimya sana

Wokovu

Couplet 1

Israeli wake Mungu, kimya sana, wa’zunguka Yeriko kwa imani. Malaika wake aliwaongoza, na waliendelea kwa kushinda.

Refrain

Twende kwa kushinda, twende kwa kushinda! Kwa Damu yake Yesu, twende kwa kushinda! Tegemea Mungu, anatuongoza, na kwa imani, twende kwa kushinda!

Couplet 2

Na Daudi, mchungaji, alikwenda mbele yake Goliathi bila woga; kwa imani alitupa jiwe lake, kwa jina lake Mungu akashinda.

Refrain

Twende kwa kushinda, twende kwa kushinda! Kwa Damu yake Yesu, twende kwa kushinda! Tegemea Mungu, anatuongoza, na kwa imani, twende kwa kushinda!

Couplet 3

Danieli aliomba kila siku, hakuhofu pango la simba kamwe; katika imani aliomba Mungu, akaokoka katika hatari.

Refrain

Twende kwa kushinda, twende kwa kushinda! Kwa Damu yake Yesu, twende kwa kushinda! Tegemea Mungu, anatuongoza, na kwa imani, twende kwa kushinda!

Couplet 4

Hata safarini huku kwenda Mbingu nikipita katika jangwa kavu, na kupatwa na ’jaribu mbalimbali, najua kwa imani nitashinda.

Refrain

Twende kwa kushinda, twende kwa kushinda! Kwa Damu yake Yesu, twende kwa kushinda! Tegemea Mungu, anatuongoza, na kwa imani, twende kwa kushinda!

Couplet 5

Na imani inashinda hali zote, inaruka juu ya mambo yote. Niliye dhaifu sitahofu kamwe, kwa kuwa Mungu ananiokoa.