#163
Ahadi zote za Mungu zinasimama
Wokovu
Couplet 1
Ahadi zote za Mungu zinasimama kweli, na zilitiwa muhuri kwa Damu yake Yesu.
Refrain
Mbingu zikiondoka, nchi ikitoweka, ’aminiye ’taona: Ahadi zinadumu.
Couplet 2
Fanya kama Ibrahimu: Uangalie juu! Nyota ukizihesabu, imani itaota.
Refrain
Mbingu zikiondoka, nchi ikitoweka, ’aminiye ’taona: Ahadi zinadumu.
Couplet 3
Katika giza njiani tutaamini tu. Muda kitambo, na tena jua litaangaa.
Refrain
Mbingu zikiondoka, nchi ikitoweka, ’aminiye ’taona: Ahadi zinadumu.
Couplet 4
Watu wakitusumbua, tutaamini tu. Yesu atusaidia majaribuni pote.
Refrain
Mbingu zikiondoka, nchi ikitoweka, ’aminiye ’taona: Ahadi zinadumu.
Couplet 5
Rafiki wakituacha, tutaamini tu. Yesu, rafiki mkubwa, atabaki daima.
Refrain
Mbingu zikiondoka, nchi ikitoweka, ’aminiye ’taona: Ahadi zinadumu.
Couplet 6
Katika mambo yo yote tutaamini tu. Tutaviona Mbinguni tulivyoviamini.