Indirimbo Zikundwa Open in the app

#165

Nitazamapo kwa imani Mwokozi

Wokovu

Couplet 1

Nitazamapo kwa imani Mwokozi wangu, nafurahi, naona utajiri wake anao Mungu, Baba yangu. Haleluya! Furaha kubwa, aniongoza siku zote! Nikiuona udhaifu, anichukuwa mikononi.

Couplet 2

Sitasumbuka mimi tena, furaha inanijaliza; Na kwa upendo na rehema anisikia, nikiomba. Haleluya! Ananitunza, Ninastarehe kwa salama. Na ukitaka raha yake, mfungulie moyo wako!

Couplet 3

Nilipokaa kati’ dhambi Nikaliona sikitiko, Lakini shaka na hukumu Zimeondoka kwangu sasa. Haleluya! Anipa nguvu Yakuyashinda majaribu. Rohoni mwangu nina raha, Nalindwa nayo siku zote.

Couplet 4

Dhihaka na mateso yote si kitu kwangu kwa sababu nafarijiwa na Mwokozi, nakumbatiwa na Babangu. Haleluya! Mwokozi wangu ananitunza kwa neema. Nikiwa na ’dhaifu tena, natiwa nguvu kwa imani.