#158
Heri mtu anaye amini Mungu Baba
Wokovu
Couplet 1
Heri mtu anayeamini Mungu Baba na Yesu Mwokozi! Heri mtu aifuataye njia nzuri ’endayo Mbinguni!
Refrain
Usifiwe, Yesu Kristo! U Mwokozi Mzuri kabisa! Usifiwe, Yesu Kristo! Bwana, nitakuona Mbinguni.
Couplet 2
Kwa furaha tunakusanyika kusikia maneno ya Mungu, na Mbinguni karibu ya Yesu tutamshangilia daima.
Refrain
Usifiwe, Yesu Kristo! U Mwokozi Mzuri kabisa! Usifiwe, Yesu Kristo! Bwana, nitakuona Mbinguni.
Couplet 3
Kuamini pasipo kuona inafaa katika safari. Siku moja atatuchukua, tutakaa milele Mbinguni.
Refrain
Usifiwe, Yesu Kristo! U Mwokozi Mzuri kabisa! Usifiwe, Yesu Kristo! Bwana, nitakuona Mbinguni.