Indirimbo Zikundwa Open in the app

#157

Haidhuru kwangu huku chini

Wokovu

Couplet 1

Haidhuru kwangu huku chini utajiri au umaskini, ila Bwana Yesu awe nami; ninatunzwa naye siku zote.

Couplet 2

Haidhuru kama ninakuta shida nyingi katika safari, ila Mchungaji wangu Mwema anilide na kuniongoza.

Couplet 3

Haidhuru kama tunakaa katika baridi au hari, kwa sababu ukombozi wetu unakaribia. Haleluya!

Couplet 4

Haidhuru kama sitapata utukufu na heshima huku; nikifanywa kama takataka, yanipasa kupendeza Bwana!

Couplet 5

Haidhuru kama njia yangu inanichokesha mara nyingi, basi, nisigombane na ndugu, na pamoja tutashangilia!

Couplet 6

Haidhuru kama tukiona sisi si wakubwa huku chini. Tuwe watumishi wake wema, na tutaingia kwake Bwana!

Couplet 7

Haidhuru kama twasafiri katika dhoruba ya bahari, kwani Yesu ni nahodha wetu, atatufikisha bandarini.