Indirimbo Zikundwa Open in the app

#156

Waliaminio neno lake Mungu

Wokovu

Couplet 1

Waliaminio neno lake Mungu watapata nguvu kuwa washindaji, kwani Bwana Yesu alituahidi atathibitisha neno kwa ishara.

Refrain

Shinda, shinda, nguvu ya kushinda! Shinda, shinda, shinda kila saa! Mungu atatupa nguvu ya kushinda, Tumtii Yesu nasi tutashinda!

Couplet 2

Kati’ vita kali tuwe na ’hodari, Mungu ndie nguvu yetu ya ajabu! Tu’amini neno: Na ishara kubwa ziatafuatana na waaminio.

Refrain

Shinda, shinda, nguvu ya kushinda! Shinda, shinda, shinda kila saa! Mungu atatupa nguvu ya kushinda, Tumtii Yesu nasi tutashinda!

Couplet 3

Nguvu ya kupiga vita ya imani, nguvu ya kupinga hila za shetani! Yesu amesema: Na ishara kubwa zitafuatana na waaminio.

Refrain

Shinda, shinda, nguvu ya kushinda! Shinda, shinda, shinda kila saa! Mungu atatupa nguvu ya kushinda, Tumtii Yesu nasi tutashinda!