Indirimbo Zikundwa Open in the app

#147

Mwenyezi Mungu wa zamani zote

Wokovu

Couplet 1

Mwenyezi Mungu wa zamani zote ni kimbilio la vizazi vyote. Katika vita anawashindia na ku’okoa watu wake wote.

Refrain

Mfalme ’kubwa ndiye Mungu, vitani anatushindia. Kwa shangwe kubwa tumsifu na tumwimbie Mungu wetu!

Couplet 2

Mwenyezi Mungu wa zamani zote aliokoa watu utumwani, kwa njia kavu katika bahari wakafikishwa ng’ambo kwa salama.

Refrain

Mfalme ’kubwa ndiye Mungu, vitani anatushindia. Kwa shangwe kubwa tumsifu na tumwimbie Mungu wetu!

Couplet 3

Mwenyezi Mungu wa zamani zote Karmeli alishinda yule Ba’li, akasikia ombi la Eliya, ’katuma Moto juu ya sadaka.

Refrain

Mfalme ’kubwa ndiye Mungu, vitani anatushindia. Kwa shangwe kubwa tumsifu na tumwimbie Mungu wetu!

Couplet 4

Mwenyezi Mungu wa zamani zote akawa naye Daudi vitani; aki’tupia jiwe Goliati, shujaa alikufa mara moja.

Refrain

Mfalme ’kubwa ndiye Mungu, vitani anatushindia. Kwa shangwe kubwa tumsifu na tumwimbie Mungu wetu!

Couplet 5

Mwenyezi Mungu wa zamani zote, uovu wote utashindwa naye. Atamseta yule mdanganyi, shetani, chini ya miguu yake.

Refrain

Mfalme ’kubwa ndiye Mungu, vitani anatushindia. Kwa shangwe kubwa tumsifu na tumwimbie Mungu wetu!

Couplet 6

Mwenyezi Mungu wa zamani zote atuongoza kwa mikono yake; anatulinda hatarini huku, Mbinguni tutafika kwa salama.