Indirimbo Zikundwa Open in the app

#146

Karibu na wenzangu nilipotea

Wokovu

Couplet 1

Karibu na wenzangu nilipotea njia, rohoni mwangu njaa, na sikuona raha, lakini sasa Yesu ni Mchungaji wangu, naandamana naye siku zote.

Couplet 2

Katika shamba lake nimefuata Yesu, ninapajua anapolisha kundi lake. Na penye maji hai napunzika sana, naona raha hapo siku zote.

Couplet 3

Lakini mchungaji apita vitu vyote, uzima aliweka kwa ’jili ya kondoo. Nikumbukapo Yesu, sioni tena kitu cha kupendeza ila yeye, Bwana.

Couplet 4

Naimba kwa furaha rohoni mwangu hivi: « Upendo wako, Yesu, ninausifu sana!» Na jina lake Yesu ni kama manukato; ananilinda vema siku zote.