Indirimbo Zikundwa Open in the app

#148

Nguvu ile ilishuka ju’ ya wanafunzi

Wokovu

Couplet 1

Nguvu ile ilishuka ju’ ya wanafunzi wote mjini mwa Yerusalem’ siku ya Pentekoste, lo! Nguvu hiyo ya Mwokozi ni sawa leo; shukuru Mungu!

Refrain

:/: Karama, karama, karama yake Mungu ni sawa hata leo, ni sawa hata leo!:/:

Couplet 2

Yesu aliwapa ahadi: «Mtapokea nguvu». Na Roho akashuka na wakamsifu Mungu. Walio wenye udhaifu, wakahubiri kwa uthabiti.

Refrain

:/: Karama, karama, karama yake Mungu ni sawa hata leo, ni sawa hata leo!:/:

Couplet 3

Roho yule aingiapo anatutia nguvu, tupate kwa imani ku’ kushinda yule mwovu. Kwa moyo wenye Moto safi tuite watu kwa Mkombozi!

Refrain

:/: Karama, karama, karama yake Mungu ni sawa hata leo, ni sawa hata leo!:/:

Couplet 4

Uingie sasa rohoni, uwashe Moto wako, tupate kusimama kwa usafi siku zote! Ufike sasa kama mbele wakati huo wa Pentecoste!

Refrain

:/: Karama, karama, karama yake Mungu ni sawa hata leo, ni sawa hata leo!:/: