Indirimbo Zikundwa Open in the app

#145

Mungu wangu mkuu wanijaza

Wokovu

Couplet 1

Mungu wangu mkuu, wanijaza mwenyewe, na uzima u katika wewe. Nina raha moyoni na amani halisi, ninaishi katika upendo.

Couplet 2

Sasa ninakusifu wewe, Yesu Mwokozi, unakaa rohoni daima. Kila ’nachohitaji wanijaza kwa pendo. Wewe yote, na mimi si kitu.

Couplet 3

Jina lako ni pendo, kulijua hakika kunafanya safari nyepesi. Mimi mtu dhaifu, ila kwako ni nguvu; niongoze katika safari!

Couplet 4

Mbele ya uso wako giza yote yatoka; nuru inaangaza moyoni. Yamepita ya kale, sasa yote ni mapya. Ni maisha ya heri ajabu!