#144
Sawa na kisima safi
Wokovu
Couplet 1
Sawa na kisima safi, chenye maji mengi, mema, ni upendo wa Mwokozi ukaao ndani yake.
Refrain
Yesu Amelifungua lango zuri la Mbinguni ili niingie humo kwa Neema yake kuu.
Couplet 2
Kama ndege awindavyo mara nyingi niliumwa, Moyo wangu ulilia, Yesu hakunifukuza.
Refrain
Yesu Amelifungua lango zuri la Mbinguni ili niingie humo kwa Neema yake kuu.
Couplet 3
Ni ajabu kubwa kweli, alinisamehe yote! Juu ya rehema yake ninaimba kwa furaha.
Refrain
Yesu Amelifungua lango zuri la Mbinguni ili niingie humo kwa Neema yake kuu.
Couplet 4
Asubuhi ya uzima nitafika mlangoni; kwa ajili ya upendo nitapata kuingia.