Indirimbo Zikundwa Open in the app

#143

Heri halisi, Yesu ni wangu

Wokovu

Couplet 1

Heri halisi, Yesu ni wangu! Yeye Mchunga, mimi ni wake. Heri yakini, yote ni heri, roho na moyo zimeokoka.

Refrain

Yesu ni wimbo na raha yangu, nitamsifu hata milele! Na nitamwona huko Mbinguni. Yesu ni wangu na mimi wake.

Couplet 2

Nilijitoa kwa Bwana Yesu, na nilipewa Wokovu wake. Huko Mbinguni kuna furaha juu ya mtu aliyetubu.

Refrain

Yesu ni wimbo na raha yangu, nitamsifu hata milele! Na nitamwona huko Mbinguni. Yesu ni wangu na mimi wake.

Couplet 3

Sasa naweza kusifu Yesu, na roho yangu inafurahi. Mimi si kitu mbele ya Mungu, bali ni heri. Namshukuru!

Refrain

Yesu ni wimbo na raha yangu, nitamsifu hata milele! Na nitamwona huko Mbinguni. Yesu ni wangu na mimi wake.

Couplet 4

Nimebatizwa katika Roho, shangwe ya Mbingu imo rohoni. Moto moyoni, pia kinywani, nashuhudia pendo la Mungu.