Indirimbo Zikundwa Open in the app

#142

Kwa namna nyingi nilitafuta

Wokovu

Couplet 1

Kwa namna nyingi nilitafuta kupata raha moyoni mwangu. Unyonge wangu haukukoma ila kwa Bwana Yesu.

Couplet 2

Na moyo wenye hatia nyingi nilimwendea Mwokozi wangu, na alinipa Wokovu wake na nguvu ya kushinda.

Couplet 3

Kwa Pendo kubwa Mwokozi wangu aliuweka uzima wake, si kitu mimi ulimwenguni, nina Wokovu kwake.

Couplet 4

Ijapo ninachukiwa huku ni mteule wa Bwana Yesu, napenda sasa kumfuata, nifike kwake Mungu!