Indirimbo Zikundwa Open in the app

#141

Mwokozi wetu anatupa Furaha

Wokovu

Couplet 1

Mwokozi wetu anatupa Furaha duniani, atuongoza kwa Neema na anatushibisha. Tazama, yupo pamoja nasi, Neema haitaisha kamwe! Haleluya, haleluya, haleluya, Amina!

Couplet 2

Ni vema kumpenda Mungu aliyetukomboa, vizuri kuwa mtu wake, sitapotea kamwe. Furaha yetu itabakia, ikiwa vyote vingetoweka. Haleluya, haleluya, haleluya, Amina!

Couplet 3

Ikiwa giza mara nyingi, na jua likifichwa, na tukijaribiwa huku twajuwa ni kwa mda. Mbinguni hatutaona kamwe huzuni wala machozi tena. Haleluya, haleluya, haleluya, Amina!

Couplet 4

Na tusisumbukie tena chakula wala nyumba, maana vyote twavipata kwa ne’ma yake Mungu. Njiani yote atuongoza aichukuwa mizingo yetu. Haleluya, haleluya, haleluya, Amina!

Couplet 5

Ikiwa vema huku chini kutegemea Yesu, furaha gani huko juu kuona uso wake. Tutaiona furaha tele, na utukufu hautaisha, Haleluya, haleluya, haleluya, Amina!