#133
Ufurahi, moyo wangu
Wokovu
Couplet 1
Ufurahi, moyo wangu, heri nyingi umepata! :/: Sikitiko limekwisha, Yesu ni wangu nami wake. :/:
Couplet 2
Ameponya roho yangu, yeye ni mponyaji Mwema; :/: Na kwa Roho ’takatifu anabatiza watu wake. :/:
Couplet 3
Jina langu ni Mbinguni, Yesu ameliandika. :/: Mimi mali ya Mwokozi hata milele na milele.:/:
Couplet 4
Na moyoni mwangu sasa ninaimba: Mungu, Baba! :/:Ni furaha kubwa sana, nina rafiki kila saa. :/:
Couplet 5
Nimeondolewa dhambi, nisitende ovu tena! :/: Kwani Yesu aokoa kila wakati na dakita. :/:
Couplet 6
Nyimbo za kusifu Mungu zinajaa Mbingu zote. :/: Moyo wangu unajibu: Amina. Mungu asifiwe» :/: