Indirimbo Zikundwa Open in the app

#132

Yesu Mwokozi, unanipenda

Wokovu

Couplet 1

Yesu Mwokozi, unanipenda, na Pendo lako ni kubwa kabisa. Ulinivuta karibu nawa, Mimi ni wako daima dawamu.

Couplet 2

Yesu Mwokozi, unanipenda, na Pendo lako lapita akili. Linanifunza kuzifahamu raha, upole na utu adili.

Couplet 3

Yesu Mwokozi, unanipenda, mimi maskini, dhaifu, mnyonge. Nimetakaswa kwa Damu yako; ninakuomba, ’nijaze upendo!

Couplet 4

Yesu Mwokozi, unanipenda, umenitilia wimbo kinywani wa kukusifu hata milele, nitakuona halisi Mbinguni.