Indirimbo Zikundwa Open in the app

#134

Watu wa Mungu, mshangilieni

Wokovu

Couplet 1

Watu wa Mungu, mshangilieni kabisa, na mwimbieni Mfalme wa Mbingu na nchi! Mungu yu nasi kwa Pendo kubwa, kamili ili tupate Wokovu.

Couplet 2

Ona ajabu! Mwokozi aliyejidhili! Pendo kamili na Neema nyingi ya Mungu: Alizaliwa, akawa mwana ADamu, atukomboe na dhambi!

Couplet 3

Sisi Wakristo tumwimbie tena pamoja Yesu Mwokozi aliye dhabihu ya kweli! Na atukuzwe hapa na huko Mbinguni, kwani alitufilia!

Couplet 4

Yesu Mfalme, kwa pendo uliniokoa, nikufuate, nikutumikie daima! Huko Mbinguni nitakusifu milele katika watakatifu.